Home » Ent. » 255 ya March 6, msanii TID, Niki Wa Pili na bodigadi wa Diamond Mwarabu Suleimani wamehusika.

Info ya kwanza kusikika kwenye 255 ya March 6, ni ishu ya bodigadi wa msanii
Diamond Plutnamz anaefahamika kama
Mwarabu Suleimani
ambae alikuwa Tajikistani kushiriki kwenye mashindano ya kupigana ya
Wrestling ambayo yalikuwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali.
Mwarabu
amesema mchezo wa kwanza alicheza na Muitaliano na game ya pili
alicheza na Muiran lakini matokeo hayakuwa mabaya tofauti na
alivyotegemea lakini siku mbili kabla ya pambano la mwisho alipata
jeraha mguuni wakati akifanya mazoezi na kupoteza michezo miwili.

Weekend hii msanii
TID kwa kushirikiana na Rader Entertainment pamoja na msanii
Nazizi kutoka Kenya watafanya show Bilz, akizungumza kwenye 255
TID
amesema amejipanga vema kwa kuwa ni show yake ya kwanza mwaka huu na
kutakuwa na wasanii mabalimbali pamoja na surprise za kutosha sambamba
na uzinduzi wa video ya msanii
Masai Sharo.

Story
ya mwisho kusikika inahusu uzinduzi uliofanyika jana wa program mpya
chini ya msimamizi wa hati miliki wa Afrika Mashariki (East African
Copyright Management) ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
January Makamba inayohusu wasanii kulipwa na vyombo vya habari vinavyocheza kazi zao, msanii
Niki Wa Pili ni miongoni mwa sananii waliohudhuria ambae amesema itasaidia msanii kupata matunda ya kazi anayoifanya.